Bookmark and Share

Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili

Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili

Image description

Muammar Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili

Muammar Al Gaddafi speaks Suaeli Kiswahili 

Audio |  |

Video |  | 

IAl-Gadhafi-Anazungumza

MUHADHARA WA KIONGOZI WAKISIASA KIFIKRA NA WANAFUNZI NA WAHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA CAMBREDGE

22.10.2007

Alianza kwa jina Allah....... akawashukuru kwa mualiko huoili azungumze nao kupitia satallite amefurahi namna wanafunzi wanavyoyapa kipaombele maswala nyeti ya wakati huu yanayoathiri jamii..kunambo yanatokea mbali na sehemu tulipo lakini yanagusa maisha yetuvizuri au vibaya,leo dunia inaelekea kuwa kijiji kimoja,kijiji hichi lazima kijiweke vizuri ili kiishi kwa amani na watu wake wajuane nakusaidiana nawasipigane nakukiharibu kijiji chao,tukitazama jua tutaona huko kuna sayari nyingi zinaelea na katika sayari yetu kunabinaadamu ambao hawaishi kwa amani kutokana nakupigana.


mmenitaka nizungumzie maswala yakimataifa kwani sisi wanaadamu tunatakiwa tutatue matatizo yetu natujuane na mageuzi ya teknolojia ya mawasiliano yametufanya tuwe karibu zaidi nakila chambali kimekua karibu. kuna matatizo mengi na mwezi huu tarehe27, mjini Sirti kunakikao cha kuzungumzia kile kinachoitwa tatizo la Darfour,nataka kuzungumzia tatizo hili liligonga majukwaa yakimataifa nakuzungumziwa kila pahala.mimi ninamtazamo wanguni muhimu kwenu wahadhiri na wanafunzi ambao mustaqbali mtakua viongozi na watoa maamuzi nchini mwenu muamko huu ni muhimu,wazo langu kwa tatizo la darfour na mlichukue katika vyombo vya habari ni kuwa swala hili nimfano wamengi yanayotokea Afrika,ni maswala yakikabila kimsingi.mnaweza kushangaa nakucheka nikikuambienieni sababu yake ni ngamia..


nasasa kuwa tatizo lakimataifa. Afrika kuna makabila elfu moja yanagombania maji na malisho na yametawanywa katika nchi khamsini nakila kabila linataka kurejea kwenye uasili wake nimatatizo yasiokwisha yatakwisha pale ustaarabu utakapokua na watu hawa kutokana na kuwanyuma kimaendeleo nakutoweka kabila nabaadae kutoweka mivutano yakikabila.kosa letu sasa nikuiingiza mivutano hiyo katika siasa ,darfour likaingia siasa..kutoka watu wanaogombania ngamia hadi kuwa lakimataifa..kuna tamaa ya nchi kuu katika eneo hili na mafuta ni sababu yakufikia hapa lilipo tatizo hili ili vikosi vyakimataifa viingiena vile vya nchi kubwa nakugawana mafuta. nguvu hizo zenye maslahi zinaweza kuwanyuma ya matatizo ya darfour,huenda hamjawahi nkuyasikia maneno haya. mimi ni peke yangu niliyeitembelea afrika kwa barabara nimekata km20elfu nikajionea wakulima nawatu katika vibanda vijijini na mijini nikakaanao,nimejionea chakula chao nanjia za maisha yao,nimejionea matatizo ya afrika tokea zama za Jomo Kenyata,Jamal Abdulnasir,Haile ssalasie,hakuna aliyepo sasa aliekuwepo kipindi hicho..

hivyo afrika naijua vilivyo.kila tatizo la afrika lisifanywe lakimataifa huko ni kutafuta hatari,kwani matatizo hayo niyakikabila. Darfour siotatizo lakisiasa,kijamii wala kiuchumi...nilakikabila,baadhi yao wakulima na wengine wachungaji napopote duniani hutokea nakumalizwa kwa mazungumza ya wenyewe kimtaa nakikabila.kwani wanamila na desturi zao,wana masultani na wafalme ..hivi hamjui kama darfour kuna wafalme na masultani wakati ni sehemu ya jamuhuri ya sudani.huu ni mfumo wetu wa kikabila na kiafrika...


nimfumo mzuri wakijamii uheshimiwe...laiti tatizo hilo lingeliwachiwa wafalme na masultani wa darfour lingekwisha. lakini kuingia nguvu rasmi ya serikali na kimataifa zikazima mchango wakijamii katika kulitatua tatizo hilo. Kwa mfano kuna watu wananjaa iwe darfori au kwengineko ,mfano darfori tatizo lilipofanywa kimataifa jumuia zakimataifa zikaanza kutoa misaada watu wakafurahia,masikini wakashukuru Mungu wakaona kumbe tatizo letu limekua lakimataifa nalinatuletea misaada hii.hivyo wanataka liendelee,nasi tumechangia kwani misaada ni kichecheo cha tatizo.watu wanajiingiza katika kambi wanadai ni wakimbizi wakichukua misaada ya umoja wamataifa mchana na usiku wanarejea majumbani mwao baada yakupata chakula kutoka katika kambi walizozijenga,hawataki tatizo liishe kwani kumalizika kwake nikutoweka misaada…nani kafungua mlango huo sisi tumeufungua..laiti kusingelikuwepo misaada..laiti tungeliwaachia wenyewe kusingelikuwepo kambi ili kujipatia misaada .


Kuna wakuu wakijadi nikimaanisha mmoja ni mwalimu ,mfanyakazi,wakili asiemaarufu,tusingempa nafasi yakuzungumza kwaniaba ya kabila au chama Fulani na idhaa zakimataifa zikimkaribisha nakusikika duniani…hii ni sifa kwake ni maradhi ya kisaikolojia kwa upande mwengine na hasa mtu anapokua alikua waziri au naibu waziri au mkuu wa mkoa au wakili au mwalimu leo anazungumza kwenye idhaa zakimataifa,akitetea wanyonge na wanaokandamizwa na maneno huenda hayana ukweli ndani yake..lakini nimambo yaliopo ndani ya nchi zinazoendelea nasio darfouri pekee,nchi za ulimwengu wa tatu zikonyuma kimaendeleo kwa sababu za ukoloni ndio kukawa na kundi hilo la walionyuma kimaendeleo na masikini.mtu huyu aliotopea na umaarufu mataifa yamtaka aje azungumze,huyu hataki tatizo lishe kwani likisha na nyota yake itazimika,hatokua na sauti atayoiambia dunia,wala kutembea kutoka dola moja hadi nyengine akizungumza na bunge la ulaya,congress ya marekani na pia anazungumza kupitia satellite.huyu atataka liendelee-kwa mfano tatizo la darfouri-litaendelea ili huyu aendelee kularaha…mimi naona tatizo kama hili lipuuzwe tusilifanye lakimataifa wala kisiasa..hili ni tatizo lakikabila liachwe.ni mivutano yakikabila nasiomwanzo kutokea ,nawenyewe husuluhishana wala dunia haisikii kwa sababu tu haukufanywa kimataifa walakisiasa….

darfouri hakuna tatizo-kama wanavyosema-tatizo la ubaguzi kati ya weusi na weupe na kati ya waarabu na waafrika..waarabu ni waafrika pia. Wasudani waarabu ni waafrika..makabila makuu ni Masaaliti,ruzeikati,zaghawa na kabila la fouri,huwezi kuwatofautisha yupi mwarabu na yupi mwafrika,wameoana ni wadini moja ya kiislamu ni wote wanafuta mdhehebu moja ya sunny,wanazungumza kiarabu na hata lahaja basi wanafahamiana.hivyo hakuna ubaguzi wakweli…kabila la masaaliti kiasili na kutoka libya katika mji wa MASLATA,likahama linazungumzwa kuwa ni lakiafrika lakini kiasili nilakiarabu…kabila la ZAGHAWA lipo libya kwa maelfu na lipo pia Tchad na Sudani..


eneo limefungamana kwa sana.RUZAIQAT lipo kusini na kaskazini mwa Darfouri nahakuna awezae kulipambanua ni lakiarabu au lakiafrika…huu ndio ukweli..ni ukweli wa huko…kuna mivutano ya wachezaji wakuu duniani mfano wa marekani na china kila mmoja anataka kuhodhi eneo na hasa linapokua lina mafuta ni hatari…kasha kuna tama ya mabeberu wanaotaka kukita miguu yao na ili kufikia hapo nilazima kuzusha mzozo waweze kuleta vikosi vyao kwakisingizio cha kulinda amani kwa nguvu..ni hatari. Samara ya mwanzo duniani…kwani utawala kiromania,kiislamu na hata kimagholi…daima wana utashi wakibeberu wakujipanua duniani nah ii inaingia darfouri.


Ama jengine lisilokua darfouri…mnatakaka tatizo lamashariki ya kati..tatizo la palestina. Nasema mimi nimwanahistoria naijua vizuri historia ya watu na eneo hili. Awali wapalestina na waisraili ni wana ndugu ..niwaasili moja..wote ni wasaamina hata lugha za kiarabu na kieburania zakaribiana.kisha kinachoitwa palestina na israili ni nyumba yapamoja..wnaweza kuishi pamoja hanahaki mmoja wao kudai eneo hilo la kati yam to na bahari ni milki yake pekee na siohaki mmoja wao kutangaza dola kwa upande mmoja.hii ni sababu ya waarabu kutoitambua kinachoitwa israili kwani waisraili wametangaza dola kwauopande mmoja juu ya ardhi ya mvutano wa pande mbili.


Mfano Cyprus,ilipotangaza kuwa ni Cyprus ya uturuki ni uturuki pekee iliyoitambua..kwanini..kwasababu pande mbili za Cyprus ya uturuki na Cyprus ya ugiriki na watu wa Cyprus..ninyumba yao ya ushirika..hakuna dola duniani inayoitambua dola hiyo lakini kwa bahati mbaya wanaitambua israili kwanini?hili ni kosa..kuna kosa tangu mwaka 1948,pale ilipotangazwa kusimama dola juu ya ardhi yenye mvutano.ni hali ambayo taratibu zinazoendelea sasa hazitatui tatizo,kwani tatizo limetumiwa vibaya mfano wa lile la darfouri,kila mmoja ameyatumia matatizo ya wapalestina na kabla ya mayahudi kwa maslahi yake..raisi anaetaka kupita katika uchaguzi..chama kinataka kushinda uchaguzi..nahata propaganda zakisiasa. Kulipokuwepo muungano wa urusi,marekani ,washirika wa farsofia na atlanti waliutumia vibaya utata wa mashariki ya kati…kwa maslahi yao..nasio kwa ajili ya wayahudi na wapalestina..


na wahanga ni wayahudi na wapalestina..wao wanapigana..wanaokufa ni wayahudi na wapalestina nasio msofieti wala mmarekani au mfaransa..mjue kama ardhi hii ni finyu sana kati ya bahari na mto jordani mji wa kalkilia una eneo la km 15 na eneo lenye watu wengi la km15 haliwezi kusimamishwa dola,ukingo wamagharibi ukijenga dola itakua telaviv namiji yote ya fukweni itakua chini yake,ukanda wa gaza upo kati ya bahari na ukingo wagharibi kwenye mto vipi iwepo dola upande mmoja upo katika bahari ya mediterenian na sehemu nyengine ipo juu ya ukingo wa mto Jordan.ndani ya israili kuna wapalestina milioni moja na baadae watakua milioni na nusu na kuendelea ..

hivyo mpaka sasa hiyo sio dola safi ya kiyahudi,namjue kuwa idadi ya wapalestina inaongezeka zaidi kuliko ile ya waisraili.wapalestina na waisraili katika dola hiyo wanaishi pamoja kwa amani ni mfano mzuri wa dola moja ya wapalestina na waisraili.kuna wapalestina wanauraia wa israili na vurugu hazitokani na hawa bali zinakuja kutoka nje ya ile ijulikanayo kama israili.eneo hili finyu la ardhi halihimili dola mbili utatuzi ni dola moja ya kidemokrasia nijuu yetu nikuushinikiza upande unaongangania ubaguzi kikabila au kilugha..nimisimamo itakayokwisha kwa wakati na isiwe kikwazo cha amani..


ni juu yao kuishi pamoja kwa amani.mjue kama mayahudi waliishi pamoja na waarabu tangu kale,na hata waarabu walipotimuliwa Hespania mnamo karne ya 15,wayahudi nao walitimuliwa na nchi zakiarabu ndio zilizowapokea wayahudi..na waromania walipoichakaza Jerusalem katika mwaka 72 hivi waliwatimua mayahudi naweakakimbilia bara arabu kwa maana waarabu ndio waliowahifadhi kutokana na ukandamizaji wa waromania kwa sababu ni wanandugu…mnajua mtume Ibrahimu A.S. ana mtoto aitwaye Ismaili ambae ni babu wa waarabu na mwanawe mwengine Is-haqa huyu ni babu wa waisraili ..


Is-haqa mwanawe ni Yaaqubu…na Yaaqubu jina lake ni Israili ambao wanaiita dola hii..ni watu wakaribu sana.mimi nimeandika kitabu cheupe kama kunakopi yakiingereza..Isratini nusu yake jina la israili na nusu ya pili palestina..lazima muwe nakitabu hiki kinaszungumzia dola moja ya wapalestina na waisraili ya kidemokrasia,mwanzo inaweza kusimamiwa na umoja wa mataifa baadae wakaachiwa wenyewe…nahakuna muhimu kama raisi awe muyahudi au mpalestina ,muislamu au mkiristo.ataechaguliwa na wananchi ndio atawale..mfano upo mbele yetu ndani ya israili kuna chama cha kiarabu na kuna wabunge wakiarabi ndani ya kenesti…nao ukingo wa magharibi ni mchanganyiko wa wapalestina na waisraili na viwanda vya israili vimejaa wafanyakazi wakipalestina kutoka ukingo wa magharibi na ukanda wa gaza na wote wanategemeana nakunamambo mengi yanayowaunganisha.


Mimi nataka dola moja nakumaliza mzozo huu..kuna masharti…kwanza: Wakimbizi wote wkipalestina waliotimuliwa tangu miaka ya 48 na 67 warejee na haki yao wananyumba zao mashamba yao na ardhi yao…pili: Dola hiyo lazima isiwe na silaha za maangamizi..hakuna dola kwenye eneo hili iwe na silaha hizo hata kama inatawaliwa na Yasir Arafat,au Mahmud Abbas. Nawaomba mkisome kitabu cheupe nimekiandika kwa lengo hili. Sasa tuje katika kuboreshwa umoja wa mataifa ambapo mmetaka mawazo yangu: Kilchokuwepo ni hamu ya kuuboresha umoja huo kwa miaka kadhaa huku tukizungumziabarasa la usalama kuongezwa idadi ya wajumbe na viti vya kudumu navisivyo vya kudumu hii sisahihi…swala ni kuurekebisha. Umoja wa mataifa si baraza la usalama ..unamaana ya jumuia kuu,baraza la usalama,mahkama yakimataifa,baraza uchumi wajamii,na baraza la himaya,unesco,unicef na fao…

na mashirika yote yaliyochini ya umoja wa mataifa. Yatokeayo sasa si demokrasia nasio kikanuni nakisheria lazima yakome..dunia lazima ibadilike.hali ya sasa niyakidikteta haihudumii amani bali inaitishia amani..baraza la amani limegeuka na kuwa lakitisho na limepora uwezo wa umoja wa mataifa na limehodhiwa na dola tano zenye haki ya turufu.nasi dola ndogo hatuna imani na baraza la amani wala umoja wa mataifa na wanamawazo wakifalsafa na wataalamu kama nyinyi wanaungana na wazo hili.dalili ya hayo ni kuvamiwa Iraq,Afghanistani na Ugoslavia na ubomoaji uliotendeka huko umefanyika kwa kuwepo umoja wa mataifa na baraza la amani..kwanini baraza hili halipitishi kifungu cha saba dhidi ya Marekani na hata Uingereza zilipoivamia Iraq bila ya haki..kwanini kwa sababu nchi hizi zina kura ya turufu..hivyo hilo sibaraza la amani..wala lakimataifa..ni baraza la wenyewe.


Tunalilia mabadiliko ya umoja wa mataifa yatakayoleta demokrasia duniani….tunaitabiri jumuia kuu(international assembly)sisi tunaiona kama bunge lakimataifa na bunge hutunga sheria nakwa hiyo ndilo lenye haki ya maamuzi ..baraza la usalama ni kama serikali mbele ya jumuia kuu,na serikali ni mtekelezaji wa maamuzi ya watungasheria. Kwa maana hivi inawezekana kwa serikali ya uingereza kutunga sheria nakulitaka bunge la nchi kuzitekeleza nikinyume chake bunge la uingereza ndilo linalotunga sheria..nakuitaka serikali kuzitekeleza.Yatokeayo sasa katika umoja wa mataifa ni kuwa serikali ambayo ni baraza la usalama ndilo linalotoa maamuzi na kanuni nakuitaka jumuia kuu ambayo ni bunge kuyatekeleza..ikimaanisha gari mbele ya punda..ni aya iliyogeuzwa. Baraza la usalama linaamua na jumuia kuu inatekeleza..!lazima iwe kinyume chake. Jumuia kuu ina ummah wote naikaitwa jumuia kuu ya umoja wa mataifa..mtaifa yote yapo katika jumuia kuu..hivyo lazima iwe na uwezo mkubwa ,hii ndio demokrasia,jumuia itakapoiadhibu nchi Fulani ,nchi hiyo itakubali ..kwanini ..


kwa sababu mataifa yote yameamua hivyo..ama kuamua nchi tano,moja au mbili nakulazimisha matakwa yao kwa nchi 14,zilizoitwa baraza la usalama,nakusema hii ndio sheria yakimataifa hii sio sheria yakimataifa hii ni batili…hii ni dhuluma na lazima ikome. Hivyo kurekebisha ni kupeleka uwezo wa baraza la usalama kwa jumuia kuu ya umoja wa mataifa na kifungu cha saba ni lazima kitekelezwe na jumuia kuu na maamuzi ya lazima yatolewe na jumuia kuu..haya ndio maamuzi ya lazima..na baraza la usalama ni juu yake kutekeleza maamuzi ya jumuia kuu..hii iwapo wanataka marekebisho ya umoja wa mataifa.Iwapo hali itaendelea hivi basi itazidi kudorora..na nchi zitajiengua kutoka umoja wa mataifa na kuanzisha jumuia kuu ya wanyonge na nyenzo yakimataifa kuporomoka.Hivi sasa nyenzo za jamii yakimataifa iliyotengenezwa imechupwa..hivi sasa kuna hati mpya ilishapitishwa..imepitishwa ikapitishwa..,ni hati mpya za umoja wa mataifa zinazosimama juu ya dhuluma na ukandamizaji. Hati ya umoja wa mataifa inakataza vitisho vya nguvu au silaha,ni mwiko kutumia nguvu au vitisho.Leo vitisho vya nguvu vinatumika kwa mwendeleo,hutumika dhidi ya yeyote yule kwa kisingizio chochote..hivyo hati ya umoja wa mataifa imekwisha.mambo yanayotokea sasa nakutokea dhidi ya Libya au Panama ,au Ugoslavia,au Iraq au Afghanistani au dhidi ya dola nyengine..ni mfano wa hati mpya ya matamshi isiyo katika maandishi ..hivyo ni lazima kuitii kanuni hii mpya..kanuni ya nguvu ,sisi tunahitaji nguvu za kanuni ya kimataifa…

kilichopo sasa ni kanuni ya nguvu za kimataifa..na ndio inayotawala nguvu za kanuni yakimataifa hivi sasa..hakuna kati yetu anaeamini kama kuna nguvu kuu zinazofanya haya na baadae kujigamba zinataka kiukweli kuzungumzia uhuru ,demokrasia na haki za binaadamu. Kama nilivyosema demokrasia lazima ifanyekazi katika kilele cha dunia,katika jumuia kuu na baraza la usalama. Demokrasia katika kitabu cha kijani natumai mnacho kwa kiingereza mnakisoma ama vipi..sio utunzi wangu pekee..kutoka kichwani mwangu tu..mimi nimekusanya majaribio ya dunia na historia ya dunia nikaona matatizo ya ndani na nje na sababu za majanga na furaha na pia sababu za ugumu na vita na pia sababu za amani.


Neno demokrasi ni asili ya lugha ya kiarabu..demo yaani wananchi na neon krasi yaani (chairs)ikimaanisha wananchi juu ya viti. Dalili yakuwa ni kutoka lugha ya kiarabu ni kwamba lugha zote wanalitamka vivyo..hivyo wananchi ni wenye haki ya kutoa maamuzi na kutunga sheria na kuweka mfumo wautakao..wao ndio mabwana..haipaswi uwezo wao uporwe ni kuwekwa katika kundi la watu liitwalo Serikali au Bunge. Mfumo wa bunge ni nadharia iliyowahadaa wananchi..nadharia inamaaana ya niaba ya wananchi..hakuna uwakilishi wa wananchi huo ni uzushi..wananchi wapo kwa nini wawakilishwe ..nani anaweza kutatua ndoto zako ..

matarajio yako na mengineyo..ni wewe peke yako unaweza kufanya hivyo. Mambo ya kisiasa kiuchumi na kijamii ni watu pekee wanayoweza kuyatenda..wanaweza kuyasemea moja kwa moja ..vipi tunakuja na mtu mmoja awawakilishe wa watu 20 elfu au laki moja na wakati mwengine milioni moja nap engine zaidi ya hapo ,mchakato huu unaonyesha wazi kuwepo ulaghai..vipi mtu huyu atawakilisha matakwa ya watu wote hao,huyu anawakilisha nafsi yake..nanyi mnaona uingereza namna wabunge wanavyofuata sera Fulani huku wananchi wakiandamana barabarani..ikiwa wabunge wanatekeleza matakwa ya wananchi kwa nini basi waandamane?

Marekani wananchi wanapinga vita dhidi ya Iraq na congress imekubali vita hiyo!!..hivyo congress haiwawakilishi wananchi.Wamarekani hivi sasa wanataka vikosi vyao viondoke Iraq na serikali haitaki kuviondosha nahakuna maamuzi katika Congress ya kuviondosha vikosi hivyo..hivyo wananchi wapo katika mkondo na mabaraza yapo mkondo mwengine..hivyo uwakilishi ni uzushi..


hivi ndio kitabu cha kijani kisemavyo..(hakuna uwakilishi wa wananchi na uwakilishi ni uzushi)..demokrasia ni mamlaka ya wananchi yaani mikutano ya wananchi na kamati za wananchi..mikutano ya wananchi ni kwamba wananchi wanagawika katika mikutano..waliowakubwa wake kwa waume wanakusanyika katika mikutano ya wananchi ambayo inaamua. Kwa mfano wananchi wa Libya wanagawika katika kata 30 elfu na kila kata ina watu 100 wake kwa waume..idadi yao ni milioni tatu..hawa wanaweza kufanya kazi za utawala Libya..waliobakia ni watoto,wasiojiweza au hawawezi kufanya kazi zakiutawala..hawa wanapanga ajenda za kazi katika jamii na sera zake za ndani na nje kwa muda wa mwaka mmoja baadae wanakutana tena….kauli mbiu daima ni ((hakuna demokrasia bila ya mikutano ya wananchi))..(( na mikutano na kamati kila pahala..

haya ni mambo mliotaka niyazungumzie natamani tukutane tena kila baada ya muda pale ninapopata nafasi..sasa kama kunamaswali au kuweka wazi jambo nipo tayari.


Swali kutoka kwa "Michael"dk wa falsafa juu ya mahusiano ya Libya: Yeye amesema kuwa amewahi kuizuru libya na kundi la wanafunzi wa cambredge nawamefurahia ziara hiyo na wameweza kujadili juu ya mageuzi ya libya hivi karibuni kuelekea mambo ya nje..na utafiti wake juu ya mahusiano ya libya na marekani na hivi karibuni kuna taarifa zakufurahisha kati ya pande mbili ili kuendeleza mahusiano hayo. "dick Tsheni" makamo wa rais wa marekani amesema:sisi tumeiangusha serikali ya Iraq na sadamu Husein yupo jela..kiongozo Gadafi Libya anafuatilia yanayotokea Iraq na Afghanistani,baada ya siku tano kukamatwa Saddam kiongozi ametangaza wazi:sisi tutaachana na silaha za maangamizi..na motto wenu Seiful islamu Gaddaf akaitikia. Mimi nasema hapa kuwa libya ilikosra ilipokubaliana na marekani..msimamo ulikua wa udhaifu kisiasa..kinyume na kuwa libya ipo katika amani kwa iliyoyafanya…kiongozi hivi unaweza kutuwekea wazi jambo lililopelekea kuboresha mahusiano na marekani na mahusiano hayo yamefikia wapi hivi sasa na muelekeo wa baadae. ----


Kiongozi : Shukran dk "Michael"…na ahsante kwa kushirikiana na walibya.ni kawaida linapotokea jambo kila mmoja hulitumia kwa maslahi yake lakini hakutangazwi wazi kabla ya kutokea nah ii hufanya wasiwasi ndani ya mchakato mzima…yaani kwa nini "Tsheni"asiyaseme hayo kabla ya Libya kuchukua maamuzi haya yakihistoria..? na kwa nini hajasema tutailazimisha Libya katika kipindi cha miezi mitano ili iache mpango wake wa nuclear..? natumeweza kufanya hivi na vile Iraq…kwa nini asiseme haya..? Anaweza..kwa sababu hivi sio ukweli..?

Amesema hivyo baada ya sisi kuchukua maamuzi haya..na baadae yeye kutafsiri atakavyo.mjue kwamba hata raisi wa marekani mwenyewe alikiri kuwa mazungumzo na Libya yaliendelea kwa miezi tisa kabla ya maamuzi haya..miezi tunazungumza kabla ya kutangaza mazungumzo hayo kati ya libya na nguvu kuu na shirika la kimataifa la nguvu za nuclear juu ya swala la kufunga mpango wa nuclear.wakati huo Sadamu Husein hajaondoshwa madarakani wala Iraq kuvamiwa .kama tungelikua tunaiogopa marekani kwa nini tuliendelea miaka thelathini na mpango huu na marekani ikiwa katika kipindi cha wazimu wa "Regani" ambae baadae aligundulika kuwa ni mwendawazimu kweli,nasi tuliwatanabahisha kuwa huyu mtu mwendawazimu wakacheka na mwishoe wakakiri na matendo yake yalikua ni matokeo ya wazimu na Henzaima.wakati huo hatukuogopa wazimu wa "Regani" akisambaza meli zake kwenye maji yetu ya kikanda na mipaka yetu lakini kwa ridhaa yetu tuliachana nayo..kila dola ilikua ikitaka kuwa na silaha za nuclear kwani ilikua ni modeli …pasi na utafiti..

tuliona mpango huu umekua wazi ,vifaa vimezuiliwa,wakaletwa makachero wa marekani na kukutana na wataalamu wa nuclear duniani na Libya ikipenya ndani ya mikutano hiyo nakuzungumza nasi kwa lugha nzuri,marekani na uingereza ,na hasa kupitia rafiki yangu "blair"..aliniletea wajumbe kadhaaa wakasema mpango umegundulika na vifaa vimekamatwa,…hapo tukahisi hatuwezi kuendelea nao…na gharama zake pia ni kubwa…kisha kwa nini tutengeneze bomu la nuclear..kwa ajili ya nani?kuna mtu atasema Libya inatengeneza bomu la nuclear ili iipige Israili hii haiwezekani kwani nilikuambieni awali hiyo iitwayo israili ndani yake ina wapalestina milioni moja..hivi kweli sisi tutapiga kombora hilo dhidi ya milioni moja ya wapalestina na wayahudi milioni tatu…


kasha ukingo wa magharibi na ukanda wa Gaza hautosalimika na kombora hili likitupwa israili kasha Syria ,Lebanoni na Jordani na hata Misri hazitosalimika na kombora hilo la Libya…ni vigumu Libya kulitumia kombora hilo katika eneo hilo..nikitu kilichombali na ukweli…sawa Libya itaipiga ulaya kwa kombora la nuclear kwa nini?..ulaya si ile yakikoloni..ulaya leo ni rafiki wa ushirika na tunashirikiana nayo katika mipango nyeti kati ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya,tunazungumzia biashara na uwekezaji na ulinzi wa mazingira na bahari ya mediterenian na mashirikiano katika taasisi za uchumi na mengineyo. Ulaya ya leo si ile ya "muselini"na zama za "Hitler"…hivyo mwenye akili hatofikiria kupigwa ulaya na nuclear kutokea Libya..ulaya ni nchi kadhaa na rafiki wa libya..nikundi jengine linaondosha uwezekano wakutengeneza nuclear kwa ajili yao..je linatengenezwa dhidi ya marekani?.

Mwanzo ili kutengeneza bomu,kutengeneza bomu libya kuipiga marekani tunahitaji mtu kati muhimu sana kulichukua hadi marekani nakulilinda kutokea libya hadi kuanguka marekani..ni kitu kigumu san asana na huenda ikawa muhali kwa nchi kama libya..na hivi inawezekana kupigwa marekani na bomu la nuclear la libya au hata mabomu kumi na marekani kujibu kwa mabomu elfu kumi..sirahisi kwa mwenye akili timamu kufikiria hivyo..atakua mwendawazimu atakaedhania kuishambulia marekani .urusi au china nchi zinazomiliki maelfu ya mabomu ya nuclear kushambuliwa na kibomu kimoja cha nuclear. Na je tutalitumia bomu hilo dhidi ya Afrika,huu ni umoja wetu na bara lrtu nasi ni sehemu yake na tunaijenga tofali baada ya tofali. Hivyo tathmini ya msimamo kimataifa ni swala lamawazo yakijadi yanakwenda na modeli ya ulimwengu,kila mmoja akiwaza kuwa nalo na baadae ukatoweka. Tumeiona Pakistani ikitengeneza bomu la nuclear ..


kwa nini ?akasema wallahi kwa ajili ya India..nayo India inasema kwa ni dhidi ya Pakistani..madamu yule analo bomu la nuclear basin a huyu pia..ni lazima na mwengine awe nalo ili kuwepo na uwiano kati yao. Kwa hakika huu ni mpango hatari sana..silaha za maangamizi ziwe za nuclear ,vijidudu au kemikali..nasi twatamani zikomeshwe..lakini kwa dunia nzima..hatumuogopi yeyote..tunamuogopa muumba pekee..uchambuzi wa "Dick Tsheni" ni sawa na wa "Regani" namuombea Mungu asiwe mgonjwa kama Regani..namuombea Mungu ampe afya..najua ni mgonjwa na amefanyiwa operesheni tano za moyo na uchambuzi wake usijeukawa ni kutokana na maradhi yake..natamani isiwe hivyo. Lakini tujaalie "Dick Tsheni"ni mkweli ni kweli nchi ndogo kama Libya yenye watu milioni tano inaweza kuingia mvutano na nguvu kuu kama Marekani,yenye kumiliki mabomu kadhaa ya nuclear na makombora yakupita mabara na meli zakubebea ndege na pia nyambizi za nuclear..hata dola ndogo ikitaka kupambana na dola beberu tatizo liko wapi?! Hii ni dalili ya hekima na ushujaa pia..hivyo kuamua kufanya hivi na kuacha kufanya vile kwa hiari yako mwenyewe ni bora kuliko kulazimishwa. --


Swali:..kiongozi mmeamua kuunda umoja wa Afrika kwenda muungano wa mataifa ya Afrika..hivi mnaamini jambo hili lingewezekana miaka kumi iliyopita au lisingeliwezekana? ------Kiongozi :

Shukran…Inawezekana sana kwa nini isiwezekane?..sisi waafrika tunajifunza kwa ulaya..na ulaya imefanyika na mataifa..mataifa yaliyokua yakipigana vita na mamilioni ya watu walikufa kwa vita hiyo ya ulimwengu ya kwanza na ya pili na vita ya wardi na vile vya miaka thelathini na vita vya miaka saba. Vita vyote hivyo waulaya wameviishi pamoja na yote ulaya imeona maslahi yake kwenye umoja..ulaya imeungana nasi kama wafrika twajifunza kwao. Juu ya hapo waafrika si mataifa yanayopigana..Afrika ni ummah mmoja mweusi wenye makabila kama nilivyosema karibu 1000…nibara moja..kundi la watu wamoja…ni rangi ya pekee nyeusi tofauti na mabara mengine..na maslahi yanatufanya tuungane..utandawazi na changamoto zake zinaifanya kila dola yakitaifa isiweze kuishi pekee.Ikiwa Ujerumani hawezi kuishi pekee isipokua kwa muungano wa ulaya au uingereza ,ufaransa na Itali..vipi Afrika na vidola vidogodogo ni maslahi zaidi kuungana ..iwe kwa umoja wa afrika au muungano wa mataifa ya afrika..lini itafikia itatokana na juhudi za waafrika wenyewe..shukran.

Swali: swali kutoka kitengo cha afrika cha "BBC",umoja wa afrika unaelekea katika muungano wa mataifa ya afrika..nasi tunahusika na umoja wa waarabu..nasi tunafurahia ushujaa wenu na hekima yenu katika umoja huu. ----

Kiongozi : Kwa hali yeyote hilo sio swali kiasi cha kutoa fikra..juu ya umoja wa waarabu ni kwamba historia ya watu hupita zama kadhaa..kuna zama za dini ..kitaifa zama za demografia au za mada.zama za dini zinafanyika na makundi ya dini bilakujali mataifa na lugha zao mfano utawala wa kiislamu na ule wakiromania ya kitakatifu mfano ya utawala wa ottoman na Abbasia….n.k Kipindi cha mataifa ni kile kilichofanyika umoja wa italic,ujerumani uturuki irani na hadi china..n.k…..kwa bahati mbaya vipindi hivi vilikua kabla ya waarabu kama taifa na hata dini moja.

 Leo ni zama nyengine,zama za demografia,zama za utandawazi na mada zinazowaunganisha wenye maslahi mamoja,ikawa ni vigumu kuzungumzia umoja kati ya libya na iraq au Syria na marakishi..leo libya na marakishi zipo katika afrika na umoja wa afrika.hivyo hakuna uwezekano wakuzungumzia umoja nje ya demografia ya afrika mfano wakuzungumzia umoja wa ulaya na newsland na Australia kwa mfano,hakuna uwezekano kwa sababu waulaya jografia imewafanya waweke umoja wao peke yao. Leo kuna Asian na dola huru za "Comman welth mpya"zilizokua chini ya muungano wa sofieti..kuna umoja wa afrika na umoja wa ulaya…


muungano wa marekani ..na marekani ya kusini inaungana…kwa maana dunia sasa inagawika makundi saba au kumi makubwa,miungano itakayokua kama dola baadae…hata sarafu zitatoweka nakubakia saba au kumi na benki kuu saba tu..dunia itakua hivi,ni vigumu kuzungumzia umoja wa kitaifa kwa waarabu mbele ya miungano hii mikubwa ambapo waarabu hawajui wapo wapi,katika muungano upi,isipokua wakiitikia wito wangu nakufanya misafara kwa ajili yake kwenye nchi za kiarabu nikizitaka zijiunge na umoja wa afrika na kuunda umoja wa waarabu na waafrika na katika hali hii waarabu wote watakua ndani ya umoja mmoja na afrika.


 Leo theluthi ya waarabu ni waafrika na theluthi nje ya afrika ipo Asia,katika bara arabu na ghuba na shamu..juu yao ni kujiunga na afrika..hatuwezi kuzungumzia umoja wa kitaifa au dini katika zama hizi kwani ni sarafu isio endana na soko la leo.Sarafu inayotumika sokoni sasa na ile ya miungano mikubwa na demografia na maslahi yakifedha mamoja…shukran. Swali : Ndugu kiongozi..mmesimama kishujaa dhidi ya udikteta na kutoa wito wa dunia iliyo na uhuru na faida kwa wote..je mmnaweza kuona msimamo juu ya iraq na marekani inayoyafanya.. ---

Dunia inajua kinachotokea Iraq na kutoa msimamo wake nahakuna utatuzi isipokua kuondokana na kosa lililotendwa..kuivamia iraq ni kosa na marekani imekiri hivyo na pia uingereza..wakasema walipata taarifa kuwa iraq inamabomu ya maangamizi..

iraq ikapekuliwa,ikagawanywa na ikapigwa mwisha ikabainika haikuwa na silaha hizo…ni jambo lakusikitisha..watu wanahilikishwa nakuchinjwa..nchi inabomolewa kwa sababu ya uvumi na uongo..kisha nchi kuu zenye viti vya kudumu kwenye baraza la usalama zinafanya hivyo hii ni hatari kubwa..

wanafanya hivyo kwa ajili ya mtu mmoja kakimbia akasema hivi na vile..ni jambo linalokera watu na dhamira ya dunia haistarehe iwapo kunaitkiwa mambo kama hayo.

Kutokana nakukiri kosa ni lazima kuondoka Iraq na kuwaachia wairaq wenyewe..shukran. Mratibu wa umoja wa wanafunzi wa cambredg katoa shukrani zake kwa kiongozi..kwa waliohudhuria…

na michango yao na juu ya wote kamshukuru kiongozi "Muammar Alkadhafi"kwa kukubali kuhudhuria nao.

 

 

Bookmark and Share