Bookmark and Share

Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili

Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili

Image description

Muammar Al Gadhafi Anazungumza - Kiswahili

Muammar Al Gaddafi speaks Suaeli Kiswahili 

Audio |  |

Video |  | 

IAl-Gadhafi-Anazungumza

MUHADHARA WA KIONGOZI KWA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA JUU YA AFRIKA KATIKA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA

16.05.2007

Kiongozi alianza kwa kuwashukuru waliohudhuria na waliotayarisha kikao hicho pamoja na walimu na wanafunzi na umoja wao......

nakuelezea matumaini yake yakuendelea vikao kama hivyo kwa ajili ya kuisaidia dunia katika kupambana na changamoto zinazokabili mabara yote kisiasa,kiuchumi na kijamii. Akasema mmenitaka nizungumzie Afrika katika karne ya ishirini na moja...natarajia maelezo yangu hayatosaidia Afrika pekee nawala sinyinyi wanafunzi wa oxford bali yaisaidie dunia nzima.


 Akasema kipindi cha nyuma kilichojulikanwa kama vita baridi nguvu kuu zilikua zikilinyang`anyia bara la Afrika,kulikua na kambi ya mashariki na ile ya magharibi na muungano wa sofieti,marekani na warso na atlantiki(NATO). Hali hii ilikuja na matokeo mabaya sana katika ngazi za kimataifa na pia Afrika. Awali Afrika iliathirika na mivutano hiyo ni ikawa ni uwanja wa mivutano ya aidiolojia na mipenyo ya kisiasa na kijeshi ya Marekani na Urusi ni mvutano wakila anaetaka kulidhibiti Bara hili na kujipatia Vibaraka wengi zaidi watakaowasaidia kupora maliasili za Afrika na kuwaburuza katika majukwaa yakimataifa,mvutano ulikua mkali sana kati ya Mashariki na Magharibi. Sisi tulikua wahanga wa mivutano hiyo,dunia haikufaidika kwani mivutano mingine iliongezeka...


kulikua na mivutano ya ulaya ya mashariki na ulaya ya magharibi nakusambaa Afrika,baadhi ya nchi za afrika zikajiunga na kambi ya mashariki na nyengine kambi ya magharibi.Afrika ikapoteza nguvu zake kama nguvu kuu zilivyopoteza nguvu zake kutokana na mivutano hiyo. Muungano wa sofiet na Marekani zikapoteza nguvu zao kwa ajili yakutaka kuhodhi pande kubwa Afrika,matokeo yakawa mabaya kwa amani ya dunia na utulivu wa dunia na pia ulinzi wa dunia pamoja na uchumi wa dunia,mapinduzi,vita,na mauaji - kiasi fulani yakatokea ulaya-mivutanona vita baridina pia vita vikali. Mambo hayo yakatokea Ulaya na pia Afrika na hasa Afrika ya kaskazini ambako mimi nipo sasa.Nakusudia kusema kuwa ikiwa kunabara linakumbwa na kinyanganyiro cha nguvu kuu iwe kinyanganyiro moto au baridi basi matokeo yake yatakua mabaya katika ngazi yakimataifa au kikanda. Hapa nataka dunia ifahamu kupitia kikao hichi nakupitia nyinyi kuchukuliwe somo kutokana na matokeo yaliyopita nakuziepuka sababu zilizopelekea matatizo hayo kutokea.

 Hapo kale ulaya iligawanyika nakulikua namapambano yakijeshi kati ya mashariki na magharibi leo ulaya imeungana na huo ni mchakato mzuri wa utulivu wakisiasa kiuchumi na kisaikolojia. Leo ulaya imekua pekee kati yake na muungano wa urusi na marekani,lazima iwe salama kwa mueko wake na isiwe eneo la mapambano. Akasema sasa naingia katika -maudhui yetu-Afrika baadfa yakumalizana na mivutano ile kwa bahati mbaya imechomoza mingine mipya ambayo inaweza kuleta majanga mapya kama yaliyopita.Afrika itakapokua uwanja wa mivutano kati ya China na Marekani kama ilivyo sasa hivyo mimi ni wajibu wangu kuwa wamwanzo kulizungumzia hilo kwani kunaaibu na kukosekana ushujaa kuzungumzia maudhui hii mfano ya mtu anaeficha maradhi mpaka yanamuumbua.Mimi sitaki kuficha ukweli huu kwa mataifa yote yawe ya afrika au mabara mingine.Kunamivutano mipya Afrika inaweza kurejesha mivutano ya kale kati ya nchi kuu.


 Mivutano hiyo itapoteza nguvu za Marekani na China ambao ndio wachezaji. Marekani imeingia afrika kwa nguvu zakijeshi na kambi zakijeshi zikitafuta nafasi Afrika nakuingilia mambo ya ndani ya Afrika kwa visingizio vya haki za binaadamu ambazo hata kwao au nchi nyingine hazipewi kipaombele. Wanazungumzia hakizabinaadamu na Demokrasia wakati huko Marekani kwenyewe na kwengineko hakuna.Wanazungumzia utawala bora na hakuna aliembora...wanaingilia undani wa mambo ya ndani ya nchi.

 Nakunapokua kunamtu kibaraka wa ukachero wa marekani akaweza kukamatwa,Marekani huanza kupiga kelele raia fulani mmemfanya nini ?wapi mmemuweka na kwanini?Hivi kuna dola inayokwenda marekani na kuiuliza serikali kwa nini raia wa marekani fulani mmemuweka ndani ?


 au kumzuru?nikitu kisichowezekana,sasa vipi marekani inajipa haki hiyo,hii ndio muingio wa marekani Afrika. Wakati China..pamoja yakua ni washindani wawili wakuu Afrika ili kuihodhi na kujifaidisha lani China uingiaji wake ni wakiulaini kwani haifuatilii utawala wa dola wala haki za binaadamu wala uhuru wakujkieleza,uandishi habari nakadhalika.Haiweki kambi zakijeshi wala haizungumzii utawala bora kwaufupi haiingilii mambo ya ndani ya nchi.China hivi sasa imeingia Afrika na zaidi ya Mashirika( 600) bali hata raia wakichina wameingia Afrika,waafrika wanawakaribisha wachina kwani muingio wao ni wakistaarabu ambao utawaletea faida nawanajiepusha namuingio wamarekani ambao unaonesha sera chafu za marekani ambazo zinawaletea hasara kama ilivyotokea Vietnamu na sasa Iraq na pia Somalia nakwengineko.sisi tunaikaribisha China tukijua nimfano wa mkoloni lakini tunamtaka mshirika dhidi ya ubabe wa marekani iwapo nayo haitotuhodhi ,iwapo tutafanya kura ya maoni kati ya nchi mbili hizo basi China itapata hii nichangamoto tunayoikabili sasa.

 Jambo jingine,ni mustaqbala wa Afrika katika umoja wa Afrika(Africa Union) iwapo Afrika itaweza kuungana hiyo ni faida kwao na dunia mfano wa umoja wa ulaya sasa umeifaidisha ulaya kama bara na pia waulaya wenyewe na pia dunia,ulaya sio tena eneo lamapambano kati ya kambi mbili.Mimi najua vikosi vya Marekanivilivyoiteka ulaya wakati wa vita ya duniabado vinaikalia ulaya,lakini swala hili lawahusu waulaya wenyewe nalinatishia amani ulaya,bahari ya mediterenian na dunia,natamani viondoke. Sasa kuna ulaya moja,sarafu moja na sera moja..haya yameleta utulivu katika dunia.


 Tunaitaka Afrika iungane pia,nakuwepo na sarafu moja ya Afrika na Benki kuu moja ya Afrika,ulinzi,Soko,uuzaji na uagiziaji mmoja na kodi ya forodha moja haya yatafaidisha uchumi wa dunia.lakini tuna nchi khamsini na sarafu khamsini na benki kuu khamsini na mifumo khamsini tofauti ya uchumi isio na uzito.uchimi wa Malawi dhidi ya Gambia na Guine bisau mbele ya block kuu hainamaana. Vipi block kama umoja wa ulaya ,Marekani,Japan au China itapoteza wakati wake kwa kuzungumza na ujumbe kutoka Gambia nini Gambia?ujumbe unataka kununua gari kumi.Lakini anapokuja kamishna wa masoko wa Afrika yote anatakakununua gari nusu milioni naam huyu ni mteja nanafaa kuzungumza nae,wananunua na kuuuza kwa bilioni......

ama Gambia ,Madagascar,Malawi, Guinea bisau au hata Libya isipokua Libya inamafuta lakini nayo ni sawa na Gambia ,Burundi,Uganda au Botswana. Lakini ulaya,marekani china au japani zitakapozungumza na waziri wa Afrika wa biashara ya nje,soko,matumizi na uuzaji nje mazungumza yatakua na bora zaidi na yenye faida kwa uchumi wa dunia. Nataka wakuu wenye ushawishi na dunia isaidie umoja wa Afrika na muungano wa mataifa ya afrika kwani vitaleta utulivu amani na usalama,kwa dunia,waafrika,ulaya na hata china na marekani. Sisi twayakaribisha mashirika ya marekani ulaya japani na china kwa lengo lakushindana kibiashara lakini sio kwa kutuhodhi kututisha au kutudharau...


hivi hatutokubali.tumeamka tunawataalamu wakiafrika na katika ngazi yakimataifa. Jambo jengine iwapo watanisikiliza wanaotumia fedha nyingi kutengeneza mabomu ya kupitiza mabara,mabomu yanuclear na kuangamiza,meli yakubeba ndege zakivita nakulishamajeshi yaliyoenea dunianilaiti sehemu ya fedha hizo wangelitupatia sisi huku Afrika,marekani china japan na ulaya wasaidiane nasi kujenga bwawa la(ANGA) nchini Congo lingezalisha umeme na Afrika yote ingelingaa na umeme kufika hadi ulaya kupitia kaskazini mwa Afrika au Asia kupitia Misri.Hivi haya ni bora au kambia za jeshi sijui utawala bora ni upi?! tusaidieni tuliokoe ziwa Tchad.tusafishe baadhi ya sehemu za mito ya congo,afrika ya kati mto shari na argoni huko cameroun ili maji kuingia ziwa Tchad kama zamani. Maneno haya yapo katika mtandao wa Alkadhafi anazungumza juu ya ziwa tchad. kuna mbavu mbili ambazo dudia inavutapumzi kupitia hizo ni misitu ya amazoni kusini mwa marekani na Congo ambazo zinakupatieni oxgen,naitaka dunia iipekipaombele namivutano inayoendelea congo inatishia ubavu huu kupatwa na jangwa. Akasema nimefurahi kugusia mambo muhimu ambayo hayajazungumziwa kabla juu ya Afrika kama kunajengine lolote mnakaribibishwa mbele yangu kuna kitabu cha kijani na kitabu cheupe,nami nakaribisha maswali yenu kwani muhadhara huu ni wachuo kikuu. ------mzungumzaji : Akamshukuru kiongozi kwa mazungumzo yake kisha akauliza kupitia mwanafunzi ,juu ya wachezaji wakuu.. kwanini hamkutumia nguvu zenu kutatua baadhi ya mivutano Afrika na kumaliza mateso yawatu kama vile Somalia na Zimbabwe? ----Kiongozi : shukran...


Wallahi mwanangu vikosi vingi vya umoja wa mataifa yawezekana robo tatu ya nne vipo Afrika,afrika kunamizozo na muhusikawake ni ukoloni ulioigawa afrika......mivutano yote niyakikabila na mipaka kati yamakabila,sisi afrika tilikua wamoja leo tuna nchi khamsini zenye mipaka iliyoingiliana.mipaka hiyo imegawa makabila nakuyakata kati ya nchi mbili na tatu. Tukiitazama cote vour na mivutano yake sababu ni kuwa watu waliokua wakiishi (upper volta)borkinafaso hivi sasa na cote vour....


 nchi mbili hizi zilikua moja ni volta ya juu ,na volta ya chini....mkoloni akazigawa....moja akaiita cote vour na nyengine akaiita volta ya juu, wenyewe wakaibadilisha nakuiita borkinafasohivyo wakaazi wakaskazini mwa cote vour wakaleta tatizo kwani sasa wamekua ni wacote vour wakiicha nchi yao nyuma,na hadi leo hawatambuliki kama wao ni raia wa cote vour yote yamesababishwa na mkoloni na tatizo bado linaendelea. Kunamaziwa makuu ambako matatizo nitija ya ukoloni kwani wamezifanya Rwanda na Burundi na Congo na makabila ya Tusi na Hotu nakujenga mivutano kati yao. Nimvutano walioijenga Congo na kumuuwa LUMUMBA na kupigania Almasi na malighafi za Congo kama urenium ili watengeneze bomu la nuclia wakaipigia Japan ,hali ni hiyohiyo Somalia ni mkoloni alieifanya Somalia ya itali na ile ya muingereza...

kwanini wasiifanye Somalia moja.......?waitali wakachukua kaskazini na waingereza kusini namakombo yao yamebakia hadi leo.....tukiitazama Gambia katika ramani nikitukisichoingia akilini...kunamto katikati ya Senegali unaitwa mto Gambia,waingereza waeuteka wakaweka dola wakawasomesha wakaazi wamto huo kiingereza wakawapa uhuru dola ikaitwa Gambia.....

dola hii imezungukwa na Senegali kila upande.....wafaransa wakaikalia Senegali.........hivyo jawabu nikua kuna vikosi vyakutosha afrika anasi ukiamua umoja wa afrika kupeleka vikosi popote pale tupo tayari lakini sikumaliza tatizo nakuleta amani...

tatizo nikubwa zaidi ya hapo.Tatizo linahitaji mafungamano ya afrika kijamii na kufyeka makombo ya ukoloni,nakuletaumoja mmoja hata nchi khamsini au wilaya elfu ndani ya mjengo mmoja wakisiasa,hapo matatizo yatakwisha.Nasi twapigania hilo,vikosi vinahitaji fedha umoja wa mataifa hautoi fedha isipokua viwe chini yake kama vile sudani inavyokataa huko Darfour.wanasema hatutaki kofia zabuluu na kupanua mamlakayake nakuweza kumkamata nakumuhukumu nakuingia kokote mfano wa marekani. swala lakupeleka vikosi hapa na pale ni gumu sana.shukran. ------Mchangio.kiongozi,mimi ni mwanafunzi wa oxford kutoka tunisia.......swali ni ju ya fikra ya umoja na demokrasia,kuna tatizo lademokrasia na tatizo la jangwa...


je wakati huoni ni mzuri kwa viongozi kulimaliza tatizo hilo..na lini itawezekana kuwanamkakati wakitaifa na kuona soko la pamoja litakalokomesha ukiritimba? Kiongozi: laiti viongozi wangesikia maneno yako nami natarajia hivyo nandio maana napigania mamlaka ya wananchi kwa maana mamlaka yawe kwa wananchi bila ya mtawala au serikali kwani hakuna chuki kati ya wananchi wa Algeria kwa mfano na wananchi wa morocco,wote ni ndugu ni wamoja,lakini kuna misimamo tofauti yakisiasa kati ya watawala.madam kuna watawala kuna siasa nawatawala wanahusika...sisi twatarajia kufikia mamlaka ya wananchi na kusimama duniani kote ili amani yakweli ipatikane duniani kote.

 wananchi hawachukiani wala hawavamiani..wavamizi ni watawala na jeshi na kutishia amani ya dunia.Tumesikia Holako,Timorilink,Jenkizkhan,Qorshi,Qambiz,Hitler,Nabilion,Mosolin,Bush na wengineo..tunasikia watu waliovamia dunia,huu ni ukweli,hao ni watawala na wanajeshi,lakini sio wananchi na hatusemi watu wa mangoli au wajerumani.

leo wajerumani wako katika amani bila ya Hitler,na alipokuwepo alitangaza vita dhidi ya ulaya na dunia. Nabilioni haina maana wafaransa ni wabaya,leo wapo katika amani lakini wakati wa nabilioni aliteka nchi kadhaa.Nami siamini kile kinachoitwa funguzi za kiarabu na kiislamu naziona ni ukoloni kwa ulaya,waarabu waliteka Saqlia mwaka 300 na kisiwa cha Aiberia mwaka 800 hawakuacha humo hata muislamu mmoja..laiti zingelikua za kiislamu kwanini maeneo hayo yasiwe yakiislamu huo siufunguzi ni uvamizi na ukoloni.

Nani aliamuru ni watawala kwa ajili ya mali...leo chaguzi na chama cha jamuhuri zinafanyika ili raisi afuzu na kuhodhi petroli yote haya ni matakwa ya watu nasio yawananchi. -----mchangio: kwa maelezo yenu umoja wa afrika unaweza kuingia kijeshi sudani bila ya wananchi wa sudani wote kukubali? --Kiongozi?kwa darfour mimi ninarai kuu katika maswala yanayotatuliwa kidiplomasia,lakini naweza kulitatua kijamii aukisaikolojia.,kwani mimi simwanadiplomasia wa mwanasiasa.,mimi ni kiongozi wa mapinduzi,ni mmboreshaji jamii,nimetumia muda mkubwa kutatua tatizi la darfour,mamia ya wazee,masultani na wakaazi wa darfour nimejadiliana nao nakutafuta utatuzi wa tatizo.lakini ikiwa kuna misaada kuna kambi za wakimbizi nawanaambiwa msiwenawasiwasi mtapata unga,mchele,maziwa na vyengine matatizo yataendeleo kwani misaada itaendelea kumiminika. Libya ilifungua njia yakupitishia misaada yakimataifa kuelekea darfour waliposikia wakaendelea namatatizo yao wakati wausiku na assubuhi wanaingia kambini kuchukua misaada na hali ni hiyo kwenye maeneo kadhaa.

Mzozo unapofanywa wakimataifa tatizo huzidi,nawakuu wakisiasa wanapopata umaarufu nakujifanya watetezi wawanyonge na dunia ikiwasikiliza inawapa kichwa nakuzidisha ugumu wautatuzi wa tatizo kwani likimaliza watajifaragua wapi nakujitapa.naona tatizo kama la darfour waachiwe wenyewe...iachiwe sudani imalize tatizo siotatizo kubwa,ukubwa umeletwa na muingilio wa nje,kunakauli kunamvutano kati ya marekani na china juu ya petroli..hivyo nguvu kuu zinatengeneza tatizo..


ni tatizo lakikoloni..nini tutafanya?. wakati china na marekani wako dhidi yako nawakati wameamua kucheza mchezo huo ili mmoja kati yao afanikiwe. ......swali jengine ni juu ya mvutano wa Palestina na Israili na mtazamo wake juu yakuutatua? kiongozi...shukrani hilo ni tatizo na ni maradhi sugu kwa dunia ,tatizo hilo limeleta pia uadui kati ya waarabu na marekani baada ya marekani kuelemea upande wa waisraili na majaribio yote yakijeshi nakiamani yameshindikana kulitatua nawachezaji wasasa wameuachamkono kwani hawanamaslahi na swala hilo.akaongeza mimi namjua mmoja wa rais mstaaf wa Italy akisema sisi twatafuta utatuzi wa wakati wetu baada ya miaka ijayo basi eneo liingie jahannam,hili ni jambo la hatari kwani baada ya daktari kuondosha maradhi kabisa anatafuta dawa yakutuliza maumivu tu na kuendelea kuteketeza mwili.

hivyo wachezaji wanalitumia swala hilo kwa maslahi yao yakuendelea katika utawala au kibiashara au kiusalama nasio kwa ajili ya tatizo asili.


 kwa mfano rais yeyote wa marekani na raisi wa sasa anapolizungumzia swala hili ni kwa min ajili ya uchaguzi achaguliwe tena naikiwa kipindi chake kimekwasha ni kwa ajili ya chama chake,kwani chama cha jamuhuri kinasema litatuliwe kwani hilo nitatizo la mashariki ya kati nawamarekani wampe kura zao...mimi simiongoni mwa wachezaji wenye maslahi katika utatuzi..sikwaajili nichagukiwe au kwa ajili ya chama au kujipigia debe,lakini baada yakuusoma mvutano huo nikaandika waraka huu ,kitabu cheupe kwa anuani"ISRATINI"Ikimaanisha Israili na Palestina,utatuzi uliomo katika kitabu hiki unaingia akilini ni ufupisho wa mawazo ya pande zote mbili,kuna wakuu na wanajeshi waliopigania kuasisi dola ya Israili wanaiona hali ya sasa ni hatari na wapalestina wanaiona vivyo....nguvu za kimataifa ni hivyo hivyo.

utatuzi wa mwisho na wakihistoria nikusimamisha dola moja kwa wapalestina na waisraili nakusimamiwa awali na umoja wa mataifa na uchaguzi usimamiwe na umoja wa mataifa...nani atashinda sio muhimu .... lazima kuondosha ubaguzi kwani wote hao ni wasami kwa maana waaarabu ni wasami na pia waisraili ni wasami kiasili ni wana wa mjomba...waisraili hawana pakwenda wanafukuzwa maeneo yote duniani,hivyo wakitakakuishi daima katika eneo hilo ni juu yao kuishi kwa amani na maingiliano kwani nguvu za marekani hazitowalinda ipo siku watajikuta kivuli cha marekani kimetoweka.ni juu yao kujiunga na upande mwengine na huo utawakubali pale watakapokua ndani ya dola moja. Ama dola khalisa ya kiisraili kwa dini lugha na ada zake haitotatua tatizo,ni mfano ya aliekua katikati ya bahari kakamata udongo usipate maji...


kwa sababu dola hii ipo katika bahari kuu ya waarabu vipi itaishi safi?kuna wapalestina milioni moja watakua milioni mbili na tatu vipi dola hiyo itaishi safi daima?hata waasisi wanaona waliofanya mwaka 48 sio utatuzi,wanangu tatizo ni kwamba pande mbili zinagombania ardhi inayoitwa palestina,mmoja anadai kaiteka nakutangaza dola kwa upande mmoja nahili ni kosa,nayo ni sababu ya waarabu kutoitambua,kwamfano wakati uturuki ilipotangaza dola ya wasaiprus wa uturuki haikutambuliwa isipokua na uturuki pekee..cyprus niyawacyprus wote..palestina ni ya wapalestina wote iwe wapalestina au waisraili,mayahudi au waislamu,waarabu au waisraili ni ya wote.hivyo ardhi hiyo haikubaki kugawiwa kwani ardhi ipo kati ya bahari namto mwembamba usiohimili dola mbili. Mayahudi duniani ni milioni 12...jaalia hao warejee katika kile kinachoitwa israili..nao wapalestina wapo milioni 5 warejee baadae watakua 6 kisha 7,jee kweli dola mbili zitaishi katika kipande kidogo cha ardhi..haiwezekani...

isratini ipo sasa ukingo wa magharibi ni mchanganyiko wa walowezi wakiisraili na miji ya wapalestina na pia ukanda wa gaza na ile ya israili ijulikanayo mwaka 48 ambako kuna wapalestina milioni moja wanabeba uraia wa israili...

wafanyakazi wakipalestina wanaendesha viwanda vya israili hivisasa..napia wapalestina wa ukingo wa magharibi na ukanda wa gaza wanafanyakazi katika ardhi ya 48,hivyo utatuzi ni dola moja kwa watu hawa,lazima kufutwa ubaguzi wa dini lugha kikabila.ni mshiko wa wakale ama vijana wa leo wakipalestina na kiisraili wanataka dola moja ,amani,utalii na biashara.hayo ndio yaliyomo kwenye kitabu cheupe nandio tatuo.wengine wanawahadaa mimi sihadai yeyote. washukran. ---------mchangio:muheshimiwa kiongozi tuelezeee mahusiano yakidiplomasia ya misri na jordani kuelekea israili...


Yasir Arafat kajenga mahusiano na israili kwajina la wapalestina,kati yenu na israili hamna matatizo,kwanini kusiwe na mahusiano yakideplomasia kati ya L ibya na Israili kama zilivyofanya nchi nyengine zakiarabu?. -------kiongozi: tulisemaje..sio swala la mahusiano..ni swala la kutatua tatizo...baada yakusema lini tatizo litatatuliwa tunasema lini tutaitambua?mbele yetu kuna tatizo...usiniambie hii nyama mbichi ya kondoo,kwa nini huili..kula ni baada yakupikwa na kukaangwa...kwanini huili..ikaange kwanza..ipike..kwanini huitambui,tutatue tatizo kwanza..tatizo bado halijatatuliwa.hili ndio swali. tatizo likitatuliwa tuulizie kutambuliwa kabla yake hakuna swali. washukran --------mchangio/mwanamke kauliza kuwa nyinyi mnamtazamo wakina juu ya maswala yakisiasa..je unanasaha zozote kwa wakuu wa Iran na Marekani juu ya matatizo kati yao?. kiongozo....ikiwa mpango wa nuclear wa irani ni kwa matumizi ya amani kwa nini wanaupinga,hawana haki.kwani irani inasema kutotumia nguvu za nuclear kwa maswala ya amani ni kuzinyima nchi za ulimwengu wa tatu kufaidika na nguvu hiyo,vipi mnatuzuia na urenium kwa maswala ya amani..ni kosa kwao kuirutubisha urenium..


ikiwa kwa amani,ikiwa kwa mambo yakijeshi kuna kauli mbili: yakwanza...Irani inaweza kusema ,iwapo dola zote zitabomoa mipango yake ya nuclear na silaha zake,nasio Libya pekee,nami nipotayari kubomoa mipango yangu ya nuclear. Ikiwa mashariki yakati ipo karibu na silaha za maangamizi karibu na irani,Pakistani inayo,India kadhalika,China na Urusi na zote zinazunguka Irani..hivyo inasema vipi mnanizuia kumiliki silaha hii na wengine wengi wanauliza kwa nini hata waarabu. inawezekana misri na Syria zikauliza baada ya israili kumiliki silaha za nuclear zikona huenda Irani ikafanya hivyo. Irani hadi sasa inadai mpango wake ni waamani na hamna haki yakunizuia. ---------Mtangazaji wa BBC/kiongozi tunakushukuru kwa niaba ya waliohudhuria hapa chuo kikuu cha Oxford tunakushukuru kwa kutupatia wakati wako na mchango na majibu yako.

 

 

Bookmark and Share